Chuo Kikuu Ardhi chawapa mwongozo wanafunzi wa shule za Sekondari

  

Chuo Kikuu Ardhi chawapa mwongozo wanafunzi wa shule za Sekondari za jiji la Dar es salaam namna wanavyoweza kujiunga na masomo ya Elimu ya juu kulingana na ufaulu wao .
 
 
 
Mtaalam wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi  akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani  kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wana uwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi na vyuo vingine leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia  kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.
 
 
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani namna ambavyo Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga mbalimbali yanayoihusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini  pia mafunzo kuhusu uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
 
 
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia na kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo jijini Dar es salaam.
 
 
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Dennis Tesha akiwaeleke za wanafunzi wa shule ya wasichana ya Jangwani namna bora kuchagua masomo yao ya baadaye kulingana na sifa walizonazo watakapotaka kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini pamoja na kazi watakazofanya mara baada ya kuhitimu kulingana na masomo yao.
 
 
Moja ya kazi ya Ubunifu wa jengo la ghorofa lilobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi.
 
 
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakifurahia jambo mara baada ya kuangalia moja ya kazi ya ubunifu wa majengo iliyofanywa na wanafunzi wa mwaka wan ne wa Chuo Kikuu Ardhi walipokuwa wakizungumza na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho Hadija Maulid leo jijini Dar es salaam.
 
 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki ya jijini Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri Msaidizi-Uhasibu na Usimamizi wa Fedha wa Chuo Kikuu Ardhi wakati wa programu maalum ya Chuo hicho ya kuwaelimisha  wanafunzi wa shule za Sekondari kuhusu masuala mbalimbali ya kitaaluma kuhusu sekta ya Ardhi yanayofundishwa na chuo hicho leo jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
Baadhi ya machapisho ya Chuo Kikuu Ardhi wakati wa Programu hiyo.
 
 
 
 
 
 
Mbunifu Majengo kutoka Chuo Kikuu Ardhi Bw. Jafer Salehe Jongo akiwafafanulia baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo hicho walioko mwaka wa nne leo jijini Dar es salaam.
 
 
 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia Machapisho kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya upimaji wa Ardhi, Uthaminishaji wa majengo, Mazingira, Mipango miji yaliyotolewa na Chuo Kikuu Ardhi leo jijini Dar es salaam wakati wa program maalum ya kuwapatia elimu waanafunzi wa shule za jiji la Dar es salaam kuhusu Chuo Kikuu A
 

Contact Us

  • homeArdhiArdhi University
  • phone(255-22) - 2771272,
    (255-22) - 2775004,
    (255-22) - 2772291/2
  • mailaru@aru.ac.tz