emblem

ARDHI UNIVERSITY

Events

Ufunguzi wa Maabara ya Kisasa

  • 29 Oct, 2021 - 13 Nov, 2021
  • Ardhi University

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi - Taaluma Prof. Gabriel Kassenga  ameambatana na mgeni rasmi Mrs. Jasmien De Winne ambaye ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Belgium Tanzania, wamefungua rasmi maabara ya kisasa ya kufundisha Teknoloji ya uendeshaji wa mitambo viwandani, iliyopo Chuo Kikuu Ardhi. Ufunguzi huo umefanyika leo tarehe 29 Oktoba,2021 

Chuo kikuu Ardhi ni moja wa wafaidika kati ya vyuo sita kutoka nchi za Tanzania, Uganda na Ethiopia chini ya Mradi unaoitwa Applied Curricula in Technology for East Africa (ACTEA)  ambapo baadhi ya washiriki katika mradi huo Chuo Kikuu Ardhi chini ya Shule ya Sayansi za Dunia, Miliki, Biashara na Infomatikia (SERBI) wameweza kupata mafunzo ya siku tano kwa lengo wa kuwajengea uwezo wa matumizi ya vifaa hivyo katika kufundisha. 

Washiriki wa mafunzo hayo ni Pamoja na wahadhiri kutoka vyuo vingine ambao nao ni wafaidika ikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe (Tanzania), Chuo Kikuu Muni, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbarara (Uganda) na Chuo Kikuu Jimma (Ethiopia).
Mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Applied Sciences and Arts (Ubeligiji).