emblem

ARDHI UNIVERSITY

News and Events

ARU Yasaini Mkataba wa Kuanza kwa Ujenzi wa Majengo Manne Kampasi Kuu DSM

 

Chuo Kikuu Ardhi kupitia mradi wa HEET kimesaini mktaba na kampuni ya ujenzi ya China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation  wa kuanza rasmi kwa ujenzi wa majengo manne (4) ambayo ni majengo ya madarasa, yenye uwezo wa  kuchukua wanafunzi 4,604,  Maabara Mtambuka (Multipurpose laboratory), yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 670, Studios, zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 780, karakana za ufundi majengo zenye uwezo wa kuchukua 492.

 Majengo hayo yote kwa jumla yatakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 6546 na walimu 93 kwa mkupuo. 

Ujenzi wa majengo hayo utakiwezesha Chuo kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 6,074 kwa sasa hadi kufikia 12,620. Udahili unaendana na maoteo ya Mpango wa Chuo (Corporate Plan) wa miaka Kumi kwa kuwa na idadi hiyo ya wanafunzi.

#Kazi Iendelee
#Weledi na Ustawi