emblem

ARDHI UNIVERSITY

News and Events

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar yapata uzoefu wa Chuo Kikuu Ardhi katika utekelezaji wa mradi wa HEET.

 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa amefanya mazungumzo na ugeni kutoka Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ulioongozwa na Mheshimiwa Mwanaisha Juma, ambaye ni Mwenyekiti akiambatana na Naibu Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Sudi Nahoda Hassan  pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo.

Aidha, Prof. Mohammed Makame Haji, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar pia aliambatana na ugeni huo. Mazungumzo hayo yana lengo la kupata uzoefu wa Chuo Kikuu Ardhi katika kutekeleza majukumu yake kwenye mradi wa HEET.

Katika majadiliano Prof. Liwa alionyesha furaha yake kwa kupokea ugeni huo na alikiri kuwa mradi wa HEET umekuwa msaada mzuri kwa Chuo Kikuu Ardhi kufikia malengo ambayo Chuo ilijiwekea katika mipango yake ya muda mrefu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati kwa niaba ya wajumbe wengine alioambatana nao alionyesha kuridhishwa na hatua zilizofikiwa na Chuo katika utekelezaji wa mradi wa HEET.

Wageni hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo la mradi ambapo kuna majengo manne makubwa yameanza kujengwa.

Ugeni huo ni fursa nzuri kwa Chuo Kikuu Ardhi katika kuimarisha mahusiano yake na Taasisi nyingine za Serikali na Vyuo Vikuu.